Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Saturday 28 January 2017

Maisha ni kupambana

Amini usiamini maisha ni kupambana ili kuwa na maisha ya furaha huna budi kupigania maisha.
Juhudi na kujituma ni silaha yako imani na subira ifanye iwe ngao yako,siku zote katika maisha huwa hapakosi changamoto na majaribu ya hapa na pale.

Tunapopata majaribu na matatizo katika maisha tusichukie bali tuyafanye kuwa somo kwetu kwani hutufanya tuwe imara zaidi na kujiongezea uwezo wa kufikiria maradufu,

Kila mwanadamu anafungu lake alilopewa na mungu na imeandikwa katika vitabu vya dini
"Mungu anampa anayejituma" hivyo basi kila mmoja wetu ni lazima ajitume ili apewe pia wahenga nao walisema "asiyefanya kazi na asile" hii inaonesha dhahiri kwamba kufanya kazi na kujituma ndio kila kitu.

Vilevile kumbuka kwamba mungu anampenda na kumruzuku mtu anayemuabudu,hivyo basi katika maisha kamwe usisahau kumuabudu mungu kwani ndiye mtoaji riziki.

Ukitaka kufanikiwa usisite kujinyima yaani kuepuka matumizi yasiyo ya lazima watu wengi hushidwa kujinyima suala linalowapelekea kushidwa kusonga mbele.jambo hili lipo sana kwa vijana ambapo wanathamini starehe kuliko kazi,

Kumbuka:uwezo wa kubadilisha maisha yako upo mikononi mwako.

No comments:

Post a Comment