Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Friday 14 April 2017

Ukweli kuhusu mafanikio

Mtaftaji wa kweli hujiuliza siku zote ukweli kuhusu mafanikio,na pia hujiuliza waliofanikiwa walipita njia gani?,haya ni maswali mhimu ya kujiuliza ukiwa kama mpambanaji wa kweli.

Amini usiamini mafanikio huanza na wewe huo ndio ukweli,utayari wako wa kutaka au kuhitaji mafanikio hayo ndio silaha pekee ya wewe kushinda hali ngumu ya maisha,utayari huo ni pamoja na kuweka niya ya dhati,siku zote ili kufanya jambo ni lazima uliwekee ya kulifanya kikamilifu
Kumbuka:penye nia pana njia.

Vilevile mafanikio huletwa na subra pamoja na uvumilivu,wengi katika maisha hukata tamaa mapema jambo ambalo ni mwiko katika upambanaji wa kupambania maisha,wengi wakiona shida zimezidi hukata tamaa na kudhani wao hawastaili mafanikio bila ya kujua mafanikio hupatwa na yule aliyevumilia na asiyekata tamaa.
Kumbuka:ukiona shida zinazidi raha inakaribia.

Mafanikio pia huletwa na uchapakazi,kamwe huwezi fanikiwa kama wewe ni nvivu wa kufanya kazi,mungu humpa yule anayejituma hivyo ni vyema kujituma ili kupata mafanikio.


No comments:

Post a Comment