Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Wednesday 3 May 2017

Kutoka milionea hadi ombaomba

Katika maisha kuna kupanda na kushuka,ukitaka kupanda lazima kujituma,ubunifu na mipango mizuri ihusike,na kushuka mara nyingi husababishwa na uzembe pia matumizi mabaya ya ulichonacho.

Katika jiji la dar es salam palikia na milionea mmoja ambaye alikua na mali nyingi sana ikiwemo kampuni mbalimbali pamoja na viwanda hapa nchini.Milionea huyo alijikuta mali zake zikipungua kadri siku zilivyosonga kwa kuwa alikua na tabia na mazoea ya kutumia pesa kiholela pasina kujua anapoteza.

Jamaa huyo alikua ni mtu wa kula bata kila siku na kujivinjari na wadada,ambapo alijikuta kwa siku anatumia hadi 700,000/= baada ya miaka mitatu alianza kujikuta anashidwa kuwalipa wafanyakazi wake na wakati mwingine alijikuta anawalipa faida yote iliyopatikana kutokana na mauzo ya kampuni yake bila kubaki hata kidogo,

Kadri siku zilivyosonga alijikuta anawalipa hadi mtaji wa kampuni,kitu kilichofanya kampuni kuyumba na kuanguka pia,kampuni nyingi za mikoani alizifunga na viwanda vilivyomo mikoani pia,alibakia na kampuni chache jijini dar.

Lakini tabia yake ya starehe haikukoma Bali aliendelea na tabia ile ile na awamu hii alikua na mawazo sana kwa kufunga kampuni zake ,ndipo marafiki walipomshauri kunywa pombe zaidi ili kupunguza mawazo,hivyo kila siku walkua wanafanya hivyo na waliongezeka yeye pamoja na marafiki zake watatu ambapo yaliongezeka matumizi Mara mbili.


Ndani ya mwaka mmoja alijikuta pia kampuni za jijini dar anashidwa kuziendesha na pia akazifunga.alibaki na nyumba pamoja na gari ya kifahari,marafiki zake walianza kumkimbia na kumuona hana maana kwao,kwa kuwa alikua mtumiaji mzuri wa pombe alishidwa kuacha akafikia hatua ya kuuza gari ili apate pesa kwa ajili ya starehe yake,

Ndani ya miezi michache hela ile ilimuishia akaamua kuuza nyumba safari hii alikua na bahati mbaya sana kwani aliporwa pesa baada ya kuuza nyumba na kubaki mikono mitupu.kwa sasa jamaa huyo ni ombaomba ndani ya jiji hilo la dar.

Dondosha comments ili twende sawa pia niambie umejifunza nini.usisite kunifolo istagram @jaysijah pia kulike page yangu ili usipitwe na mambo kama haya..

No comments:

Post a Comment