Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Saturday 13 May 2017

Faida za kufanya nazoezi ya mwili

Kuwa na afya bora ni msingi wa mafanikio yote. Hata uwe na mipango na malengo mazuri vipi  kama afya yako ni mbovu huwezi kuyafikiwa mafanikio hayo unayoyataka. Unapokuwa na afya bora inakuwa inakupa nguvu ya kuishi maisha bora wakati wote na kufanya mambo mengi bila kutetereka.

Kama unaishi maisha ya kulakula hovyo tu bila utaratibu kamwe usitegemee ikawa rahisi kujenga afya bora ni lazima itakusumbua. Vilevile hata kama hujihusishi na mazoezi nayo pia itakuwa ni tatizo kwa afya yako. Ili ufanikiwe ni muhimu kutambua kitu cha kwanza kukilinda ni afya kuliko kitu chochote kile.

Kwa hiyo utakuja kuona kuwa chakula bora chenye virutubisho vyote muhimu, ni kitu cha lazima na msingi sana kwa afya zetu. Mbali na vyakula hivyo pia hata mazoezi yanahusika pia katika kutupa afya nzuri


Zijue faida za kufanya mazoezi

1. Mazoezi ya mwili husaidia kupunguza shinikizo la damu.

2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto.

3. Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).

4. Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi.
5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili. 
6. Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo 
7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.

Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili.

No comments:

Post a Comment