Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Friday 5 May 2017

Shilole mbioni kuvaa shela

star wa kike kutoka Bongofleva Shilole maarufu kama ‘Shishi Baby’ amebainisha kuwa yupo mbioni kuvaa shela baada ya kupata mchumba ambaye anampenda kwa dhati na tayari amemtambulisha kwao.

Star huyo amesema ndoa yake itafanyikia ndani ya uwanja wa taifa

Shilole amesema mchumba wake huyo ni mwenyeji wa Arusha na anatamani hiyo siku ya ndoa kila mtu ahudhurie. Pia shilole kafunguka kwa kusema "Nataka ndoa yangu kila mtu ahudhurie, nijaze uwanja wa Taifa. Ndoa itafungwa juu ya ndege tutashukia uwanja wa Taifa"

Hata hivyo Shilole amesisitiza kuwa amekuwa akificha mahusiano yake akihofia kuyaweka wazi kwa sababu hata mahusiano yake ya awali yalivunjika kutokana na kuwekwa zaidi hadharani: “Mahusiano yangu ya nyuma yalivunjika kwa sababu niliyaweka wazi kwa watu wa karibu. Kwa sasa, namficha mume wangu mtarajiwa.”

No comments:

Post a Comment