Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Friday 5 May 2017

Stev nyerere ataja sababu za kuanguka kwa bongo movie

Tasnia ya filamu tanzania yaporomoka kwa kiwango kikubwa na kuzua mizozo kati ya wasinii wao kwa wao pia wasanii wa muziki na wasanii wa filamu,

Baada ya kuporomoka kwa tasnia hiyo serikali imeliangalia suala hilo na kuanza kulichukulia hatua,ambapo imeamua kupiga marufuku filamu za njee kuingia ili filamu za ndani ziuze.

Suala hilo limeibua migogoro baina ya machinga wanaouza movie za nje pamoja na wasanii wa filamu za ndani,

Stev nyerere amefunguka kwa kusema mambo yanayosababisha filamu za bongo kuanguka ni pamoja na ubinafsi uliopo kwa wasanii husika,pia upendo kati yao haupo vilevile ushirikiano kati yao ni mdogo.

Stev nyerere ameamini hayo ni mambo yanayosababisha bongo movie iporomoke na ili bongo movie ipande tena lazima vitu hivyo vilivyotajwa hapo viwepo ili kuiinua bongo movie.

No comments:

Post a Comment