Nimekusogezea habari za Tanzania na nje ya tanzania,pia story zote za mastaa wa bongo na njee ya bongo, "Ungana na mimi jaysijah uhabarike"

Breaking

Monday 8 May 2017

Mambo yanayosababisha hali ngumu ya maisha

Katika maisha kuna vitu vipo kwa lengo la kukukwamisha usipae kimaendeleo,vitu hivyo hisababishwa na kujiendekeza kwa mtu husika.vitu hivyo ni kama vile

1)uvivu:
Siku zote mvivu hawezi fanikiwa kwani mambo yake huyapeleka kivivu na kushidwa kabisa kupiga hatua kimaendeleo.
Kumbuka:imeandikwa kila mmoja atakula kwa jasho.

2)anasa:
Vitu kama pombe,mirungi na starehe zingine zisizokua na maana,ni mambo yanayokumalizia pesa na kujikuta badala ya kusonga mbele wewe unarudi nyuma

Kumbuka:pombe,mrungi nk ni adui wa mafanikio

3)kutokujiamini:
Uoga wa kujaribu ni kansa inayokushusha kimafanikio na kukufanya usiendelee kabisa,ni vyema kujaribu na sio kuogopa.

Kumbuka:uoga wako ni kushidwa kwako.


No comments:

Post a Comment